Ilichapishwa: Julai 30, 2024
Kuanza Kutumika: Septemba 30, 2024
Masharti haya ("Masharti") husimamia matumizi ya bidhaa, tovuti na huduma hizo za watumiaji wa Microsoft zilizoorodheshwa mwishoni mwa Masharti haya hapa (http://approjects.co.za/?big=servicesagreement#serviceslist) ("Huduma"). Unakubali Masharti haya kwa kufungua akaunti ya Microsoft, kupitia matumizi yako ya Huduma, au kwa kuendelea kutumia Huduma baada ya kuarifiwa kuhusu mabadiliko ya Masharti haya.
1. Faragha Yako. Faragha yako ni muhimu kwetu. Tafadhali soma Taarifa ya Faragha ya Microsoft (https://go.microsoft.com/fwlink/?LinkId=521839) ("Taarifa ya Faragha") kama inavyofafanua aina za data tunazokusanya kutoka kwako na vifaa vyako ("Data"), jinsi tunavyotumia Data yako, na misingi ya kisheria tuliyo nayo ili kuchakata Data yako. Taarifa ya Faragha pia inaeleza jinsi Microsoft inavyotumia maudhui yako, ambayo ni mawasiliano yako na wengine; machapisho yaliyowasilishwa na wewe kwa Microsoft kupitia Huduma; na faili, picha, hati, sauti, kazi za kidijitali, mitiririko ya moja kwa moja na video unazopakia, hifadhi, tangaza, unda, zalisha au unazoshiriki kupitia Huduma, au maingizo unayowasilisha ili kuzalisha maudhui ("Maudhui Yako"). Ambapo uchakataji unategemea idhini na kwa kadri inayoruhusiwa na sheria, kwa kukubali Sheria na Masharti haya, unatoa idhini kwa Microsoft kukusanya, kutumia na kufichua Maudhui na Data yako kama ilivyofafanuliwa katika Taarifa ya Faragha. Katika hali nyingine, tutakupa notisi tofauti na kuomba idhini yako kama iliyorejelewa katika Taarifa ya Faragha.
2. Maudhui Yako. Huduma zetu nyingi hukuruhusu kuunda, kuhifadhi au kushiriki Maudhui Yako au kupokea nyenzo kutoka kwa wengine. Hatudai umiliki wa Maudhui Yako. Maudhui yako yanasalia kuwa yako na unawajibika kwayo.
3. Kanuni ya Maadili. Unawajibika kwa maadili na maudhui yako unapotumia Huduma.
4. Kutumia Huduma na Usaidizi.
5. Kutumia Programu na Huduma za Wahusika Wengine. Huenda Huduma zikakuruhusu kufikia au kupata bidhaa, huduma, tovuti, viungo, maudhui, nyenzo, michezo, ujuzi, ujumuishaji, boti au programu kutoka kwa wahusika wengine huru (makampuni au watu ambao sio Microsoft) ("Programu na Huduma za Wahusika wengine"). Huduma zetu nyingi pia hukusaidia kupata, kufanya maombi, au kuingiliana na Programu na Huduma za Wahusika Wengine na zinaweza kukuruhusu au kukuhitaji kushiriki Maudhui au Data Yako na Programu na Huduma za Wahusika Wengine, na unaelewa kuwa kwa kutumia Huduma zetu unazielekeza zikuwasilishie Programu na Huduma za Watu Wengine. Programu na Huduma za Wahusika Wengine zinaweza kukuruhusu au kukuhitaji uhifadhi Maudhui au Data Yako kwa mchapishaji, mtoa huduma au mwendeshaji wa Programu na Huduma za Wahusika Wengine hao. Huenda Programu na Huduma za Wahusika Wengine zikakupa sera ya faragha au zikahitaji ukubali masharti yao kabla uweze kusakinisha au kutumia Programu au Huduma za Wahusika Wengine. Angalia sehemu ya 13.b kwa masharti ya ziada ya programu zinazopatikana kupitia Maduka mengine yanayomilikiwa au kuendesha na Microsoft au washirika wake (ikiwa ni pamoja na, lakini haijakomea kwa, Office Store, Microsoft Store kwenye Xbox na Microsoft Store kwenye Windows. Unastahili kuhakiki masharti na sera za faragha ya wahusika wengine kabla ya kupata, kutumia, kuomba, au kuunganisha Akaunti yako ya Microsoft kwenye Programu na Huduma zozote za Wahusika wengine. Masharti yoyote ya wahusika wengine hayarekebishi Masharti haya. Microsoft haikupi leseni ya rasilimali yoyote ya akili kama sehemu ya Programu na Huduma yoyote ya Wahusika wengine. Unakubali kuwajibika kwa hatari na dhima zote zinazotokana na matumizi yako ya Programu na Huduma hizi za Wahusika Wengine na kwamba Microsoft haitawajibika kwa matatizo yoyote yanayotokana na matumizi yake. Microsoft haitawajibika kwako au wengine kwa maelezo au huduma zinazotolewa na Programu na Huduma zozote za Wahusika Wengine.
6. Upatikanaji wa Huduma.
7. Visasisho vya Huduma au Programu, na Mabadiliko kwa Masharti Haya.
8. Leseni ya Programu. Isipokuwa iwe pamoja na makubaliano tofauti ya leseni ya Microsoft (kwa mfano, ikiwa unatumia programu ya Microsoft ambayo imejumuishwa na ni sehemu ya Windows, basi Masharti ya Leseni ya Programu za Microsoft ya Mfumo wa Uendeshaji wa Windows husimamia programu), programu yoyote inayotolewa na sisi kwako kama sehemu ya Huduma hutegemea Masharti haya. Programu zinazopatikana kupitia Maduka mengine yanayomilikiwa au kuendeshwa na Microsoft au washirika wake (ikiwa ni pamoja na, lakini haijakomea kwa Office Store, Microsoft Store kwenye Windows na Microsoft Store kwenye Xbox) hutegemea sehemu ya 13.b.i hapa chini.
9. Masharti ya Malipo. Ikiwa ulinunua Huduma, basi masharti haya ya malipo yanatumika kwa ununuzi wako na unakubaliana nayo.
10. Huluki Inayotoa Mkataba, Chaguo la Kisheria, na Eneo la Kutatua Mizozo. Kwa matumizi yako ya Huduma zisizolipishwa na zinazolipishwa zenye chapa ya Skype, ikiwa unaishi nje ya Ulaya, Mashariki ya Kati na Afrika, una mkataba na, na marejeleo yote ya "Microsoft" katika Masharti haya humaanisha, Skype Communications S.à.r.l, 23 – 29 Rives de Clausen, L-2165 Luxembourg isipokuwa kama imebainishwa vinginevyo hapa chini. Kwa Huduma zisizolipishwa au zinazolipishwa za watumiaji zenye chapa ya Skype, ikiwa unaishi nje ya Ulaya, Mashariki ya Kati na Afrika, Sheria ya Lasembagi husimamia utafsiri wa Masharti haya na madai ya ukiukaji, haijalishi mgongano wa kanuni za kisheria. Sheria za mkoa au nchi unayoishi husimamia madai yale mengine yote (ikiwa ni pamoja na kuwalinda wateja, ushindani usio wa haki, na madai ya kosa la daawa). Ikiwa unaishi nje ya Ulaya, Mashariki ya Kati na Afrika, wewe na sisi tunakubali kwa mamlaka ya kipekee na mahali pa mahakama ya Lasembagi kwa mizozo yote inayoibuka au inayohusiana na Masharti haya au Huduma za watumiaji zenye chapa ya Skype. Kwa Huduma nyingine zote, huluki ambayo unaingia katika mkataba nalo, sheria husika, na eneo la kutatua mizozo linatokea hapa chini:
Huenda sheria za watumiaji za eneo lako zikahitaji baadhi ya sheria za eneo lako kusimamia au kukupa haki ya kutatua mizozo katika mdahalao mwingine licha ya Masharti haya. Ikiwa ni hivyo, chaguo la sheria na matoleo ya mdahalo katika sehemu ya 10 hutumika kulingana na jinsi sheria za watumiaji za eneo lako zinaruhusu.
11. Waranti.
Pia una haki ya kuchagua fidia au kubadilishwa kwa matatizo makubwa na bidhaa. Ikiwa tatizo la bidhaa au huduma halichukuliwi kuwa tatizo kubwa, una haki ya tatizo hilo kurekebishwa kwa muda unaofaa. Ikiwa hii hataifanywa una haki ya fidia ya bidhaa na kukatisha mkataba wa huduma na kupata fidia ya sehemu yoyote isiyotumiwa. Pia una haki ya kufidiwa kwa hasara au uharibifu wowote unaoweza kutabiriwa unaotakana na matatizo ya bidhaa au huduma.
12. Kikomo cha Dhima.
13. Masharti Maalum ya Huduma. Masharti kabla na baada ya sehemu 13 hutumika kwa ujumla kwa Huduma zote. Sehemu hii ina masharti maalum ya huduma ambayo ni nyongeza ya masharti ya jumla. Masharti haya maalum ya huduma yanasimamia ikiwa kuna migongano yoyote na masharti ya jumla.
14. Mchanganyiko. Sehemu hii, na sehemu za 1, 9 (kwa viwango vilivyopatikana kabla ya mwisho wa Masharti haya), 10, 11, 12, 15, 17 na zile kwa masharti yake zinatumika baada ya Masharti haya kuisha zitaponea usitishaji au ukatishaji wa makubaliano haya. Kwa kiasi kinachoruhusiwa na sheria husika, huenda tukatumia Masharti haya, tukatoa mkataba mwingine wa majukumu yetu chini ya Masharti haya, au kutoa leseni nyingine ya masharti yetu chini ya Masharti haya, ikiwa yote au sehemu yake, wakati wowote bila kukupa ilani. Huwezi kupangia Masharti haya au kuhamisha haki zozote za kutumia Huduma. Haya ndiyo makubaliano yote kati yako na Microsoft kwa matumizi yako ya Huduma. Yamechukua nafasi ya makubaliano yote ya mapema kati yako na Microsoft kuhusiana na matumizi yako ya Huduma. Kwa kukubaliana na Masharti haya, hujategemea taarifa, uwakilishaji, waranti, ufahamu, shughuli, ahadi au thibitisho lolote kando na lililowekwa hapa moja kwa moja katika Masharti haya. Sehemu zote za Masharti haya yanatumika kwa upeo unaoruhusiwa na sheria husika. Ikiwa mahakama au msuluhishi itasema kwamba hatuwezi kutekeleza sehemu ya Masharti haya kama ilivyoandikwa, tunaweza kubadilisha maneno hayo na maneno mengine kama hayo kwa kiwango kinachoweza kutekelezwa chini ya sheria husika, lakini salio lingine la Masharti halitabadilika. Masharti haya ni ya kukunufaisha wewe na sisi tu. Masharti haya si ya kumfaidi mtu mwingine, isipokuwa warithi na wateuliwa wa Microsoft. Vichwa vya sehemu ni vya marejeo tu na havina athari ya kisheria.
15. Madai Lazima Yawasilishwe Ndani ya Mwaka Mmoja. Madai yoyote yanayohusiana na Masharti au Huduma hizi lazima yawasilishwe mahakamani (au usuluhishi ikiwa sehemu ya 10.d inatumika) ndani ya mwaka mmoja wa tarehe ambayo ungeweza kuwasilisha madai kwa mara ya kwanza, isipokuwa sheria yako ya nchini iwe inahitaji muda zaidi wa kuwasilisha madai. Ikwia hayajawasilishwa ndani ya muda huo, basi huzuiliwa kabisa.
16. Sheria za Biasharanje. Lazima ufuate sheria na masharti yote ya nyumbani na ya kimataifa ya biasharanje ambayo yanatumika kwa programu na/au Huduma, ambazo zinajumuisha vizuizi vya mwisho, watumiaji, na matumizi. Kwa maelezo zaidi kuhusu vizuizi vya kijiografia na biasharanje, tembelea http://approjects.co.za/?big=exporting.
17. Kuhifadhi Haki na Majibu. Isipokuwa kama ilivyotolewa moja kwa moja chini ya Masharti haya, Microsoft haikupatii leseni au haki nyingine za aina yoyote chini ya hataza yoyote, jinsi ya kujua, hakimiliki, siri za biashara, alama za biashara au mali yoyote ya akili inayomilikiwa au kudhibitiwa na Microsoft au chombo chochote husika, ikiwa ni pamoja na lakini haijakomea kwa jina lolote, alama ya biashara, nembo au yoyote kama hiyo. Ukipatia Microsoft wazo, pendekezo, au majibu yoyote, ikiwa ni pamoja na lakini bila kukomea kwa mawazo ya bidhaa, teknolojia, matangazo, majina ya bidhaa, majibu ya bidhaa na maboresho mapya ya bidhaa (""Majibu""), utayapatia Microsoft, bila gharama, mirabaha au majukumu mengine kwako, haki ya kutengeneza, yaliyotengenezwa, kuunda kazi ya wengine, kutumia, kushiriki na kufanya biashara na Majibu yako kwa njia yoyote na kwa lengo lolote. Hutatoa Majibu ambayo yanategemea leseni ambayo inahitaji Microsoft kutoa leseni ya programu, teknolojia au nyaraka zake kwa mhusika mwingine yeyote kwa sababu Microsoft hujumuisha Majibu yake ndani yake.
Notisi na utaratibu wa kufanya madai ya ukiukaji wa haki za uvumbuzi. Microsoft inaheshimu haki za uvumbuzu za wahusika wengine. Ikiwa ungependa kutuma arifa ya ukiukaji wa haki za uvumbuzi, ikiwa ni pamoja na madai ya ukiukaji wa hakimiliki, tafadhali tumia taratibu zetu za kuwasilisha Arifa za Ukiukaji (http://approjects.co.za/?big=en-us/legal/intellectualproperty/infringement) ni taratibu zipi zinaunda sehemu ya Masharti haya. MASWALI YANAYOHUSIANA TU NA UTARATIBU HUU NDIYO YATAPATA MAJIBU.
Microsoft hutumia michakato iliyowekwa katika Kichwa cha 17, Sheria za Marekani, Sehemu ya 512, na, inapohitajika, Sura ya Tatu ya Kanuni (EU) 2022/2065, kujibu arifa za ukiukaji wa hakimiliki. Katika hali zinazofaa, huenda Microsoft ikalemaza au kusitisha pia akaunti za watumiaji wa huduma za Microsoft ambao wanaendelea na ukiukaji. Zaidi ya hayo, katika hali zinazofaa, Microsoft inaweza kusimamisha arifa za uchakataji kutoka kwa watu binafsi au mashirika ambayo mara kwa mara hutuma arifa zisizo na msingi. Ufafanuzi zaidi wa taratibu zinazotumika kwa Huduma fulani, ikijumuisha urekebishaji unaowezekana kwa maamuzi yaliyochukuliwa na Microsoft kama sehemu ya taratibu hizi, yanaweza kupatikana kwenye Arifa za Ukiukaji (http://approjects.co.za/?big=legal/intellectualproperty/infringement).
Arifa na taratibu kuhusu masuala ya mali miliki katika utangazaji. Tafadhali hakiki Maelekezo yetu ya Mali Miliki (https://go.microsoft.com/fwlink/?LinkId=243207) kuhusu masuala ya mali miliki kwenye mtandao wetu wa utangazaji.
Arifa za hakimiliki na chapa za biashara. Huduma hizo ni hakimiliki ©Microsoft Corporation na/au wasambazaji wake, One Microsoft Way, Redmond, WA 98052, U.S.A. Haki zote zimehifadhiwa. Masharti hayo yanajumuisha Miongozo ya Biashara na Chapa ya Microsoft (http://approjects.co.za/?big=en-us/legal/intellectualproperty/trademarks/usage/general.aspx) (kama ilivyorekebishwa mara kwa mara). Microsoft na majina, nembo, na ikoni za bidhaa, programu, na huduma zote za Microsoft huenda ni alama ambazo hazijasajiliwa au zimesajiliwa za makampuni ya Microsoft nchini Marekani na/au mamlaka mengine. Ifuatayo ni orodha isiyo kamili ya chapa za biashara za Microsoft kwenye http://approjects.co.za/?big=en-us/legal/intellectualproperty/trademarks/EN-US.aspx. Majina ya makampuni na bidhaa halisi yanaweza kuwa chapa za biashara za wamiliki husika. Haki zozote ambazo hazijatolewa moja kwa moja katika Masharti haya zimehifadhiwa. Programu fulani inayotumiwa katika seva fulani za tovuti za Microsoft inategemea kwa kiasi fulani kazi ya Kikundi Huru cha JPEG. Copyright © 1991-1996 Thomas G. Lane. Haki zote zimehifadhiwa. Programu ya "gnuplot" inayotumiwa katika seva fulani za tovuti za Microsoft ni hakimiliki ya © 1986‑1993 Thomas Williams, Colin Kelley. Haki zote zimehifadhiwa.
Arifa ya kimatibabu. Microsoft haitoi ushauri wa kimatibabu au wa huduma yoyote ile ya afya, utambuzi au matibabu. Daima tafuta ushauri wa daktari wako au mtoa huduma mwingine wa afya aliyehitimu ukiwa na maswali yoyote kuhusiana na hali ya kimatibabu, lishe, mazoezi au mpango wa afya. Kamwe usipuuze ushauri wa mtaalamu wa kimatibabu au kuchelewa kuutafuta kwa sababu ya maelezo uliyoyafikia kwenye au kupitia Huduma.
Manukuu ya hisa na data ya violezo (pamoja na thamani za violezo). Habari za kifedha zinazotolewa kupitia Huduma ni kwa matumizi yako ya kibinafsi yasiyo ya kibiashara pekee. Huwezi kutumia data au alama zozote za kifedha za mtoa leseni yeyote wa tatu kuhusiana na utoaji, uundaji, ufadhili, biashara, elimusoko, au matangazo ya vifaa vya kifedha au bidhaa za uwekezaji (kwa mfano, vielezo, unyambuaji, bidhaa zilizopangwa, hazina ya uwekezaji, hazina ya ubadilishanaji fedha, uwekezaji, n.k., ambapo bei, faida na/au utendakazi wa kifaa au bidhaa ya uwekezaji inategemea, inahusiana, au imekusudiwa kufuatilia data yoyote ya kifedha) bila mkataba tofauti ulioandikwa, na mtoa leseni wa tatu.
Arifa ya kifedha. Microsoft sio dalali/wakala au mshauri aliyesajiliwa wa uwekezaji chini ya sheria za amana za serikali ya Marekani au sheria ya amana za mamlaka mengine na haitoi ushauri kwa watu kuhusu ushauri wa uwekezaji, ununuzi, au uuzaji wa amana au bidhaa au huduma nyingine za kifedha. Hakuna chochote kilicho kwenye Huduma hizi ni ofa au ombi la kununua au kuuza amana yoyote. Microsoft au watoa leseni wake wa manukuu ya hisa au data ya violezo hawaidhinishi au kupendekeza bidhaa au huduma zozote maalum za kifedha. Hakuna chochote katika Huduma kimekusudiwa kuwa ushauri wa kitaalamu, ikiwa ni pamoja na, lakini haijakomea kwa, ushauri wa uwekezaji au ushuru.
Arifa kuhusu Viwango vya Video vya H.264/AVC na VC-1. Huenda programu ikajumuisha teknolojia ya kodeki ya H.264/AVC na/au VC-1 iliyotolewa leseni na MPEG LA, L.L.C. Teknolojia hii ni umbizo la ufinyazi wa data wa maelezo ya video. MPEG LA, L.L.C. inahitaji arifa hii:
BIDHAA HII INA LESENI CHINI YA HATAZA YA H.264/AVC NA VC-1 KWA MATUMIZI BINAFSI NA YASIYO YA KIBIASHARA KWA MTUMIAJI (A) KUSIMBA VIDEO KULINGANA NA VIWANGO VYA ("VIWANGO VYA VIDEO") NA/AU (B) KUSIMBUA VIDEO YA H.264/AVC, MPEG-4 YA KUONA, NA VIDEO YA VC-1 AMBAYO ILISIMBWA NA MTUMIAJI ANAYEHUSIKA KATIKA SHUGHULI BINAFSI NA ISIYO YA KIBIASHARA NA/AU ILIPATIKANA KUTOKA KWA MTOA VIDEO MWENYE LESENI YA KUTOA VIDEO KAMA HIYO. HAKUNA LESENI ILIYOTOLEWA AU ITAKAYODOKEZWA KWA MATUMIZI MENGINE YOYOTE. MAELEZO YA ZIADA YANAWEZA KUPATIKANA KUTOKA KWA MPEG LA, L.L.C. ANGALIA TOVUTI YA MPEG LA (https://www.mpegla.com).
Kwa malengo ya ufafanuzi tu, arifa hii haizuii au kukataza matumizi ya programu iliyotolewa chini ya Masharti haya kwa matumizi ya biashara ya kawaida ambayo ni ya kibinafsi kwa biashara hiyo ambayo haijumuishi (i) usambazaji upya wa programu kwa wahusika wengine, au (ii) uundaji wa nyenzo zenye teknolojia zinazoafikiana na VIWANGO VYA VIDEO kwa usambazaji kwa wahusika wengine.
Arifa kuhusu Kiwango cha Video cha H.265/HEVC. Huenda programu ikajumuisha teknolojia ya usimbaji ya H.265/HEVC. Access Advance LLC inahitaji arifa hii:
IKIWA ITAJUMUISHWA, TEKNOLOJIA YA H.265/HEVC KATIKA PROGRAMU HII IMESHUGHULIKIWA NA MOJA AU ZAIDI YA MADAI YA HATAZA ZA HEVC ZILIZOORODHESHWA KATIKA: PATENTLIST.ACCESSADVANCE.COM. KULINGANA NA JINSI ULIVYOPATA PROGRAMU, HUENDA BIDHAA HII IKAWA NA LESENI CHINI YA ORODHA YA HATAZA ZA MAPEMA ZA HEVC.
Ikiwa programu hii imesakinishwa katika kifaa cha Microsoft, habari za ziada za leseni zinaweza kupatikana katika: aka.ms/HEVCVirtualPatentMarking.
MASHARTI YA LESENI YA PROGRAMU YA KAWAIDA
MICROSOFT STORE, MICROSOFT STORE KWENYE WINDOWS, NA MICROSOFT STORE KWENYE XBOX
Masharti haya ya leseni ni makubaliano kati yako na mchapishaji wa programu. Tafadhali yasome. Hutumika kwenye programu unazopakua kutoka Microsoft Store, Microsoft Store katika Windows au Microsoft Store katika Xbox (kila moja inayorejelewa katika masharti haya ya leseni kama "Store"), ikiwemo masasisho au nyongeza zozote za programu, isipokuwa programu ije na masharti tofauti, ambapo masharti hayo hutumika.
KWA KUPAKUA AU KUTUMIA PROGRAMU, AU KUJARIBU KUFANYA YOYOTE KATI YA HIZI, UNAKUBALI MASHARTI HAYA. UKIKOSA KUYAKUBALI, HUNA HAKI NA HUSTAHILI KUPAKUA AU KUTUMIA PROGRAMU.
Mchapishaji wa programu inamaanisha shirika linalokupa leseni, kama ilivyobainishwa katika Store.
Ukifuata masharti haya ya leseni, huna haki zilizo hapa chini.
Kizuizi hiki kinatumika kwa:
Hutumia pia hata kama:
Bidhaa, programu na huduma zifuatazo zimeshughulikiwa na Makubaliano ya Huduma za Microsoft, lakini huenda zisipatikane katika soko lako.